Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:47, 19 Novemba 2024 (UTC)Reply

Masahihisho Katika makala

hariri

Habari ndugu @Christina Charles na kupongeza kwa kujitahidi kuhariri katika wikipedia yetu ya kiswahili, Nasisitiza kupitia masahihisho yanayofanywa na wakaguzi kwenye makala zako ili kuepuka kurudia makosa yaleyale kila mara. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 08:57, 21 Novemba 2024 (UTC)Reply

Asante, ndugu Justine Msechu naomba msaada wakunielewesha zaidi juu ya hayo masahihisho ili niweze kutungeneza makala bora zaidi.Amani kwako Christina Charles (majadiliano) 10:53, 21 Novemba 2024 (UTC)Reply
Ukienda kwenye makala husika Uliyoianzisha upande wa kulia juu kuna mahali pameandikwa View history apo utaona ni watu wangambi wamerekebisha makala yako na ni nini hasa wamebadilisha chukulia mfano link hii (https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kyle_Porter&action=history) Justine Msechu (majadiliano) 13:25, 21 Novemba 2024 (UTC)Reply
Ndugu naona bado unarudia makosa yaleyale, embu fwatilia masahihisho yanayofanywa ilikujifunza zaidi, ama kama bado kunakitu uelewi wasiliana nami kupitia barua pepe yangu ili tuelekezane zaidi. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 09:05, 23 Novemba 2024 (UTC)Reply
Shida bado ileile. Angalia masahihisho tunayolazimisha kukufanyia. Kwa nini usiweke mabano unapoweka tarehe ya kuzaliwa mwanzoni? Kwa nini uache tarehe nje ya mwezi wake? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:06, 24 Novemba 2024 (UTC)Reply
Kwa kuwa husikii wala kujibu, nakuzuia kwa siku 1 kwanza. Ni kama unafanya makosa kwa makusudi ili kutusumbua sisi kuyasahihisha. Unapoweka siku ya mwezi katika mabano kiungo kinaleta mwaka! Kwa mfano 26 Julai, inasoma 26 ni mwaka 26 BK. Jaribu kuona. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:36, 27 Novemba 2024 (UTC)Reply
Habari, Samahani kwa kurudia makosa kwa kutokuelewa kwangu mimi ni mgeni katika kuhariri makala ninajitahidi kujirekebisha naomba kuondolewa zuio nililo wekewa . Asante Christina Charles (majadiliano) 15:28, 28 Novemba 2024 (UTC)Reply
Mbona zuio lilikuwa la siku moja tu? Uko huru kuendelea na uchangiaji, tena tunakushukuru. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:07, 29 Novemba 2024 (UTC)Reply
Asante nashukuru Christina Charles (majadiliano) 14:00, 29 Novemba 2024 (UTC)Reply
Naona maendeleo, ila wanaume usiwaweke katika jamii ya wachezaji wanawake! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:59, 2 Desemba 2024 (UTC)Reply
Wanamuziki kawaida si wachezaji mpira! Usiwawekee kigezo:mbegu-cheza-mpira ila kigezo:mbegu-mwanamuziki. Vilevile katika jamii.

Pia uelewe kigezo {{BD}}. Ni hivi: {{BD|Mwaka wa kuzaliwa, yaani, 1958|usiweke kitu - ila kama mtu kafa weka mwaka aliokufa, yaani, 2009}}

Chumba cha kwanza mwaka wa kuzaliwa tu Chumba cha pili mwaka aliokufa ANGALIZO Usiweke jamii yoyote kama vile: "waliozaliwa", "waliofariki", na "watu walio hai". Ukiweka {{BD|1950|}} - katika jamii itataja "waliozaliwa 1950" na "watu walio hai". {{BD|1950|2012}} - katika jamii itataja "waliozaliwa 1950" na "waliofariki 2012". Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:29, 5 Desemba 2024 (UTC)Reply

habari ndugu hongera na uandishi kuwa makina punguza mwendo kuna makala hujaandika kitu ndani na umechapicha bila kitu Bruce Cockburn Hussein m mmbaga (majadiliano) 07:25, 12 Desemba 2024 (UTC)Reply
asante kwa kurekebisha Hussein m mmbaga (majadiliano) 08:07, 12 Desemba 2024 (UTC)Reply
Pongezi kwa kwenda kasi na kwa kukwepa makosa ya awali, ila bado kuna hatua nyingine: kwa mfano kuacha Kiingereza katika kichwa cha makala (singer, musicians, n.k.). Kweli hujui kutafsiri maneno hayo? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:19, 13 Desemba 2024 (UTC)Reply

Ukurasa wa mtumiaji

hariri

Mpendwa Christina,

Inashauriwa kuunda ukurasa wa mtumiaji ili kufahamiana zaidi. Karibu sana na pongezi kwa kazi nyingi. MuddybLonga 05:43, 11 Januari 2025 (UTC)Reply

Bonnie Zimmerman

hariri

Ni kheri ungeendelea na makala zako fupifupi zinakuwa hazina kokoro. Kitendo cha kuandika full length article with that kind of uharibifu kwa kweli it's completely unacceptable. Usitumie mashine kwa makala ndefu inaleta mkanganyiko mkubwa wa kisarufi. MuddybLonga 07:53, 22 Machi 2025 (UTC)Reply

Makala fupi sana zisizo onyesha umuhimu

hariri

Mpendwa Christina,

Inashauriwa kuandika makala ndefu kidogo zinazo onyesha maana ya ulichokiandika au umuhumu acha kuandika makala fupi, sio bora. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 15:57, 17 Agosti 2025 (UTC)Reply

Jihae Kim

hariri

Hi Christina, you have created the article Jihae. You give her year of birth as 1974 with an archived Variety article from Wayback Machine (here) as the source. However it seems that this article from 2016 has never mentioned her date of birth and gave her age at the time as 27, supporting her current claim to have been born in 1989. I do know that 1974 is her correct date of birth - but do you maybe know another, citable source for this, please? --KnightMove (majadiliano) 19:50, 1 Septemba 2025 (UTC)Reply

Mwanasiasa

hariri

Dada, mtu anaweza kuwa mwanasiasa, si siasa! Usibadilishe vigezo ovyo, tafadhali! Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:21, 18 Septemba 2025 (UTC)Reply

Habari , samahani sijaelewa Christina Charles (majadiliano) 14:36, 18 Septemba 2025 (UTC)Reply
Yaani katika makala juu ya mtu fulani uliweka kigezo:mbegu-siasa. Nilikisahihisha kwa kuandika kigezo:mbegu-mwanasiasa. Kumbe ukakirudisha kuwa kigezo:mbegu-siasa. Labda hukutambua ulichofanya. Lakini unaendelea kutunga makala za watu kwa kuweka chini kigezo:mbegu-siasa. Sahihi ni kigezo:mbegu-mwanasiasa. Tena, kama ni Mtanzania ni afadhali uweke kigezo:mbegu-mwanasiasa-Tanzania, ni kama ni Mkenya uweke kigezo:mbegu-mwanasiasa-Kenya mradi tuna vigezo vya pekee vilivyoboreshwa jana. Endelea na juhudi zako, tafadhali. Kwa jumla unakwenda vizuri. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:21, 19 Septemba 2025 (UTC)Reply
Kwa kweli anahitaji pongezi kwa juhudi. Czeus25 Masele (majadiliano) 12:29, 19 Septemba 2025 (UTC)Reply
Habari, asante kwakunielewesha sikuwa nimeelewa masahihisho ila ulivyonijuza ndipo nikakagua nakutambua wapi nilipokosea... Asante na .Samahani sana . Christina Charles (majadiliano) 16:54, 20 Septemba 2025 (UTC)Reply

Tuzo - Kuanzisha Makala mpya

hariri

Ninakukabidhi Tuzo ya Uhariri ya Wikipedia kwa juhudi zako za kuanzisha makala mpya! Czeus25 Masele (majadiliano) 12:32, 19 Septemba 2025 (UTC)Reply

Habari, Asante yakushukuru. Christina Charles (majadiliano) 16:49, 20 Septemba 2025 (UTC)Reply

Mbegu

hariri

Dada, hongera sana kwa maendeleo yako. Hata hivyo usichoke kujifunza zaidi, hasa kwa kupitia mabadiliko ya makala zako mpya tunayoyafanya. Kwa mfano, ni vizuri unapoweka {{mbegu-mwanasiasa}} kwa Mkenya uiongeze na kuandika {{mbegu-mwanasiasa-Kenya}}. Ni vilevile kwa Mtanzania. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:04, 27 Februari 2026 (UTC)Reply

Habari,Asante kushukuru ... Nikutakie kazi njema na siku njema Amani Itawale Christina Charles (majadiliano) 12:39, 27 Februari 2026 (UTC)Reply
Dada, tafadhali tumia tahajia Moroko badala ya Morocco. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:19, 28 Machi 2026 (UTC)Reply
Habari,samahani kiongozi unazungumzia nibadili kwenye makala nzima au. Christina Charles (majadiliano) 13:24, 28 Machi 2026 (UTC)Reply
Yaani tahajia ya Kiswahili ni Moroko, ya Kiingereza ni Morocco. Katika jamii unatumia Moroko, lakini katika makala yenyewe umetumia mara nyingi Morocco. Sasa kwenda kubadilisha katika makala zote ni kazi kubwa. Ndiyo sababu nimekushtua. Asante kwa ushirikiano! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:50, 28 Machi 2026 (UTC)Reply
asante nashukuru, Nafurahi sana pale unaponirekebisha. Nisamehe na pia usinichoke maana ndio nayidi kujifunza taratibu. Christina Charles (majadiliano) 15:04, 28 Machi 2026 (UTC)Reply
habari , samahani nimerekebisha Christina Charles (majadiliano) 07:44, 29 Machi 2026 (UTC)Reply

Jamii

hariri

Dada, unapoweka jamii uwe makini zaidi. Watu wote wa Kanada unawawekea [[jamii:Waimbaji wa Kanada]]... Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:25, 10 Agosti 2026 (UTC)Reply

Hujasoma hayo? Mbona unaendelea kuita waimbaji watu wasio na sifa hiyo? Natarajia utarekebisha makala zako za karibuni kuhusu watu wa Kanada. Asante. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:17, 10 Agosti 2026 (UTC)Reply
Habari, samahani sijaelewa naiwekaje ikiwa hivyo Christina Charles (majadiliano) 12:07, 10 Agosti 2026 (UTC)Reply
sawa samahani pia nimepitea ulizosahihisha nikapata mwangaza wa unachonielekeza Christina Charles (majadiliano) 12:22, 10 Agosti 2026 (UTC)Reply

Kupitia masahihisho

hariri

Dada, pamoja na kuendelea kwa bidii, naomba upitie masahihisho yangu: mambo mengi ni yaleyale: kwa mfano, unaweka "amezaliwa" kwa mtu aliyekwishakufa! Pia French Canadian maana yake ni Mkanada anayetumia Kifaransa, si mtu wa Ufaransa na Kanada. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:35, 19 Agosti 2026 (UTC)Reply

Tafadhali, dada, usinipotezee muda mwingi kurekebisha yaleyale... Angalia masahihisho ya makala zako ili ujifunze zaidi, la sivyo itanibidi kukusimamisha kidogo kwanza. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:32, 27 Agosti 2026 (UTC)Reply
Habari, Pole nna hongera kwa kazi. samahani najitahidi kuwa makini kiongozi wangu na kujikagua dah nisamehe tu kiongozi... nisamehe mimi maana sijuii hata kwanini nisamehe mimi Christina Charles (majadiliano) 16:30, 27 Agosti 2026 (UTC)Reply
Pole kwa kutoelewa. Nilitoa mfano mmoja hapo juu: ukisema "fulani amezaliwa" maana yake bado yu hai. Sahihi ni kusema "alizaliwa". Lakini mwanzoni, karibu na jina, tunapoweka mabano hatuandiki kwamba alizaliwa na alifariki, ila tunaweza tarehe zake tu. Halafu baada ya tarehe hatuwezi mkato kabla ya mwaka. Pia pengine katika jamii unaweza "mwigizaji filamu wa Kanada", kumbe alizaliwa huko, lakini makala inasema ni raia wa Uingereza au Marekani... Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:12, 28 Agosti 2026 (UTC)Reply
habari. Hongera na poule na kazi, asante na samahani mimi nilijua ni kwenye marejeo kumbe ni kenye kuandika makala mwanzo kabisa.
hi bado sijaelewa "mwigizaji filamu wa Kanada", kumbe alizaliwa huko, lakini makala inasema ni raia wa Uingereza au Marekani... Christina Charles (majadiliano) 09:13, 28 Agosti 2026 (UTC)Reply
Usiogope: kuuliza si ujinga! Umetengeneza kurasa nyingi kuhusu watu wa Kanada, lakini baadhi yao hawakuwa raia wa nchi hiyo, labda walizaliwa huko au walifanya kazi huko. Basi, katika jamii uandike nchi za uraia wao. Pia mara nyingine uliandika katika jamii kwamba ni mwigizaji filamu, kumbe ni mwanamuziki. Kazi njema na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:45, 28 Agosti 2026 (UTC)Reply
sawa naomba niendelee kuandika nikirekebisha. nisamehe na usinichokee Christina Charles (majadiliano) 10:05, 28 Agosti 2026 (UTC)Reply
Habari ndugu hongera na pole nimekusaidia kurekebisha makala uliyo anzisha Georgie Collins na umeandika kifupi sana na umetaja tu tarehe yakuzaliwa na mahali anapoishi pamoja na kazi hata sentensi haieleweki unapochagua kuanzisha makala jitahidi kuandika kitu msomaji mwingine akisoma aweze kuelewa , amani kwako Hussein m mmbaga (majadiliano) 09:47, 31 Agosti 2026 (UTC)Reply
asante kushukuru Christina Charles (majadiliano) 09:59, 31 Agosti 2026 (UTC)Reply
Dada, naona hatujaelewana kuhusu mabano ya mwanzoni mwa makala ya mtu. Kama hajafa, tunaandika "amezaliwa" kabla ya tarehe au mwaka, ila kama ameshafariki, ni wazi kwamba tarehe ya kwanza ni ya kuzaliwa, na ya pili ni ya kufariki, hivi hatuandiki "alizaliwa" wala "amefariki". Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:48, 10 Septemba 2026 (UTC)Reply
Habari Kaka. Asante nashukuru, mimi nilijua ni kote atuandiki. Christina Charles (majadiliano) 09:53, 10 Septemba 2026 (UTC)Reply