Rula
Rula (kutoka Kiingereza ruler) ni kifaa kinachotumika kupima urefu wa kitu na kuchora. Kizio cha kawaida cha kupima urefu ni Mita (m).

Hata hivyo, mita si kizio pekee cha kupima urefu, kuna vizio vingine kama vile Kilometa, sentimeta, Milimita na vilevile Maili n.k. ambavyo hutumika kupima urefu.[1]
Aina
haririHistoria
hariri
Rula zilianza kutumika miaka mingi iliyopita. Ufito wa shaba wa kupimia wa kale kabisa ni wa mwaka 2650 KK na ulivumbuliwa na Mjerumani Eckhard Unger huko Nippur.[2][3][4]
Rula zilizotengenezwa kwa pembe ya ndovu zilitumiwa kwenye Ustaarabu wa Bonde la Indus kabla ya 1500 KK. Rula ya aina hii ilipatikana wakati wa uchimbaji huko Lothal (2400 KK) ikiwa na milimita 1.6.
Anton Ullrich alivumbua rula ya kukunja mwaka 1851. Frank Hunt alivumbua rula inayopindika mwaka 1902.[5]
Marejeo
hariri- ↑ "ruler noun - Definition, pictures, pronunciation and usage notes - Oxford Advanced Learner's Dictionary at OxfordLearnersDictionaries.com". www.oxfordlearnersdictionaries.com. Archived from the original on 25 October 2017. Retrieved 25 April 2018.
- ↑ Engineering Toolbox. "Rollers and Bearings – Uses and Applications". https://www.engineeringtoolbox.com
- ↑ Autoevolution. "Rollers and their Applications in Automobiles". https://www.autoevolution.com
- ↑ Machine Design. "How Rollers Work in Manufacturing Processes". https://www.machinedesign.com
- ↑ "Flexible Ruler Invented by Frank G. Hunt". National Museum of National History. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |