Historia ya sayansi na teknolojia
Historia ya sayansi na teknolojia ni fani ya historia inayochunguza maendeleo ya uelewa wa ulimwengu wa asili (sayansi) na uwezo wa mwanadamu kuibadilisha (teknolojia) katika nyakati tofauti. Taaluma hii pia inachunguza muktadha wa kitamaduni, kiuchumi, na kisiasa na athari za mienendo ya kisayansi; inaweza pia kuchunguza matokeo ya teknolojia mpya kwenye nyanja za kisayansi zilizopo.

Utafiti wa kitaaluma kuhusu historia ya sayansi
haririHistoria ya sayansi ni fani ya kitaaluma yenye jumuiya ya kimataifa ya wataalamu. Mashirika makuu ya kitaaluma ya fani hii ni pamoja na Jumuiya ya Historia ya Sayansi, Jumuiya ya Uingereza ya Historia ya Sayansi, na Jumuiya ya Ulaya ya Historia ya Sayansi.
Masomo mengi ya historia ya sayansi yamejikita kujibu maswali kuhusu sayansi ni nini, jinsi inavyofanya kazi, na ikiwa inaonyesha mwelekeo na ruwaza ya kiwango kikubwa.[1]
Historia ya masomo ya kitaaluma ya historia ya sayansi
haririHistoria za sayansi awali ziliandikwa na wanasayansi wanaofanya kazi na wale waliostaafu,[2] kuanzia hasa na kitabu William Whewell, History of the Inductive Sciences (1837), kama njia ya kuwasilisha fadhila za sayansi kwa umma.[3]
Auguste Comte alipendekeza kwamba kunapaswa kuwe na taaluma maalum ya kushughulikia historia ya sayansi.[4]
Ukuaji wa taaluma mahususi ya historia ya sayansi na teknolojia haukutokea hadi mwanzoni mwa karne ya 20.[5] Wana historia wamedokeza kwamba hili liliambatana na mabadiliko ya jukumu la sayansi katika kipindi hichohicho.[6]
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, rasilimali nyingi ziliwekwa katika kufundisha na kufanya utafiti wa taaluma hiyo, kwa matumaini kwamba ingesaidia umma kuelewa vizuri Sayansi na Teknolojia, huku zikianza kuchukua nafasi muhimu sana duniani.[7]
Kwenye miongo kadhaa tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, historia ya sayansi iligeuka kuwa taaluma, ikiwa na shule za uzamili, taasisi za utafiti, udhamini wa umma na wa kibinafsi, majarida yanayokaguliwa na wataalamu, na vyama vya kitaalamu.[8]
Marejeo
hariri- ↑ What is this thing called science?. Hackett Pub. 1999. ISBN 978-0-87220-452-2.
- ↑ Reingold, Nathan (1986). "History of Science Today, 1. Uniformity as Hidden Diversity: History of Science in the United States, 1980-1960". British Journal for the History of Science. 19 (3): 243–262. doi:10.1017/S0007087400023268. S2CID 145350145.
- ↑ Snyder, Laura J. (2023), Zalta, Edward N.; Nodelman, Uri (eds.), "William Whewell", The Stanford Encyclopedia of Philosophy (Winter 2023 ed.), Metaphysics Research Lab, Stanford University, retrieved 2025-03-09
- ↑ Bourdeau, Michel (2023). "Auguste Comte". The Stanford Encyclopedia of Philosophy. Metaphysics Research Lab, Stanford University. Retrieved 15 October 2023.
- ↑ "Historiography of science - Acemap". ddescholar.acemap.info. Retrieved 2025-06-28.
- ↑ "Historiography of science - Acemap". ddescholar.acemap.info. Retrieved 2025-06-28.
- ↑ Katzir, Shaul (2017). ""In war or in peace:" The technological promise of science following the First World War". Centaurus. 59 (3): 223–237. doi:10.1111/1600-0498.12161. ISSN 1600-0498.
- ↑ Hoopes, James; Ross, Dorothy (1992). "The Origins of American Social Science". Journal of Interdisciplinary History. 22 (3): 536. doi:10.2307/205020. ISSN 0022-1953.